Diamond na Rayvanny Waomba Msamaha BASATA na Serikali Baada Ya Kufungiwa.


Wasanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka Katika Label ya WCB Diamond Platnumz na Rayvanny ameibuka na kuomba Radhi kwa serikali na BASATA siku chache Baada ya kufungiwa.

Wiki iliyopita Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) walitangaza kuwafungia wasanii Diamond Platnumz na Rayvanny Baada ya kukaidi amri yao na Kuperfom wimbo wa Mwanza uliofungiwa kwenye tamasha lao la Wasafi Festival.

BASATA Walitangaza kulifungia tamasha la Wasafi Festival na pia kuwataka wasanii hao kutoperfom katika nchi nyingine yoyote pamoja na kwamba walishapanga kwenda Kuperfom Nchini Kenya. Lakini Wasanii hao wameomba msamaha Kwa BASATA na Serikali kwa ujumla na kuomba wasemehewe adhabu yao waliyopewa.

 VIDEO

0 Comments

Previous Post Next Post