Wastara Akosolewa Kujianika Adharani Kipindi Hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Wastara Akosolewa Kujianika Adharani Kipindi Hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

MREMBO mkongwe wa Bongo Movies, Wastara Juma, amekosolewa kwa kitendo chake cha kujianika mitandaoni akiwa ameshikilia tasbii anaswali.Licha ya kuweka picha hiyo kwa nia njema ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani katika ukurasa wake wa Instagram, baadhi ya watu walimkosoa kwa kumtaka afanye jambo hilo bila kujionesha lakini pia wengine walimpongeza.“Sasa wewe unaswali ama unaonyesha watu kama mcha Mungu ama kuna matangazo ya kuswali hapo umechemsha… kila kitu Instagram hee unacheza  wewe,” aliandika jamaa mwenye akaunti iitwayo Mbwenitegg.Hata hivyo, wachangiaji wengine katika picha hiyo walionekana kumsifia kwa kumcha Mungu wake kwani amefanya hivyo ili ikiwezekana na wengine wajifunze kuswali kupitia yeye. Alipotafutwa Wastara kuhusu hilo, simu yake haikupatikana. 

0 Comments

Previous Post Next Post