“UDF ni zaidi ya vyama vya siasa” - ZittoKiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe Akizungumzia ushirikiano huo wa kidemokrasia (DeFront), Zitto anasema hilo ni vuguvugu litakalohusisha si vyama vya siasa tu, bali makundi mbalimbali katika jamii.


Akizungumza na eatv.tv Zitto amefunguka kuwa Chama cha ACT Wazalendo Katika kikao chake cha Kamati Kuu cha Januari Mwaka 2018 kiliazimia kuwa ni muhimu kujenga mashirikiano na vyama vingine na makundi mengine ya kijamii.

“Tunataka kujenga ‘The Democratic Front’ kwa kuhusisha wana Demokrasia nchini kwa madhumuni ya  kutetea, kuimarisha na kulinda demokrasia yetu ya vyama vingi pia kujenga Uchumi shirikishi wa Wananchi”, amesema Zitto

Zitto anafafanua kuwa tayari chama chake kimeanza mazungumzo na vyama vya siasa, asasi za kiraia na vyama vya wafanyakazi ili kufikia azma hiyo. 

0 Comments

Previous Post Next Post