TANZIA: Mwanamuziki Sam wa Ukweli afariki dunia, Mtu wake wa Karibu Afunguka

.Msanii Sam wa Ukweli Afariki Dunia

Msanii wa Bongo Fleva, Sam wa Ukweli amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Juni 7, 2018 baada ya kuugua na mwili wake kupelekwa katika hospital ya Mwananyamala.

Taarifa hiyo imethibitishwa na msambazaji wa nyimbo zake na Meneja wa ‘Team Mtaa kwa Mtaa’, Amri the Business ambaye aneeleza kwa masikitiko makubwa kuwa Sam amefariki dunia na kumtakia kupumzika kwa amani.

“Siamini kilichotokea muda huu ila sina jinsi, kwani woote safari ni moja, pumzika kwa amani Sam wa Ukweli, hakika nilikupenda kama ndugu yangu wakuzaliwa tumbo moja, #rip” amesema Amri the Business.

Pia, aliyekuwa mtayarishaji wa nyimbo za Sam wa Ukweli, Steve amesema Sam alikuwa akiumwa na walipomuuliza alisema ni UKIMWI wa kulogwa.


0 Comments

Previous Post Next Post