Simba Ipo Vizuri Sasa Kuja na Tuzo Zake Maalum Mo Dewji Simba Awards

Simba Ipo Vizuri Sasa Kuja na Tuzo Zake Maalum  Mo Dewji Simba Awards

Mfanyabiashara maarufu Tanzania ambaye pia ni muwekezaji kwenye klabu ya Simba, leo ametangaza rasmi kuwa ameanzisha tuzo maalumu kwa klabu hiyo.


Tuzo hizo ambazo amezipa jina la MO Simba Awards zitatolewa Juni 11, 2018 katika hoteli ya Hyatt Regency na zitakuwa na vipengele 16 ambavyo vimelenga mashabiki, wachezaji na viongozi wa klabu hiyo.

Kwenye Taarifa aliyoitoa kwa vyombo vya habari akizungumzia lengo hasa la tuzo hizo, MO Dewji amesema kuwa “Simba ni timu kubwa inastahili kuwa na tuzo zake ambazo zitakuwa zinatolewa kwa kutambua mchango wa wenzetu ambao umetuwezesha kupata mafanikio haya ikiwepo kushinda taji la Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Ni jambo ambalo litawatia moyo kuendelea kujituma lakini hata kwa ambao watakosa itawatia hamasa na hivyo kuongeza juhudi”.

Vipengele vitakavyogombaniwa ni Mhamasishaji Bora wa Mwaka na Tawi Bora la Mwaka, Kiongozi Bora wa Mwaka, Tuzo ya Wasimamizi wa Mchakato wa Mabadiliko, Mhamasishaji Bora wa Mwaka kwenye Mitandao ya Kijamii na washindi watapatikana kwa kupiga kura kwenye website ya mosimbaawards.co.tz . 

0 تعليقات

أحدث أقدم