Nipo Bize na Maandalizi ya Kumpokea Wifi Yangu Zari- Esma

po Bize na Maandalizi ya Kumpokea Wifi Yangu Zari- Esma

DADA wa staa wa Afro- Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnamuz’, Esma Khan ‘Esma Platnumz’ amefunguka kuwa, mwezi huu wote yupo bize kumsubiri mzazi mwenza wa kaka yake huyo ambaye ni wifi yake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.

Akizungumza na na Over Ze Weekend, Esma alisema kuwa, hawezi kuielezea furaha aliyonayo juu ya kurejea tena kwa Zari ambaye walikuwa hawajamuona kwa muda mrefu kutokana na matatizo ya hapa na pale na kaka yake huyo.

“Sijui nisemeje, yaani Madale (Tegeta, Dar, nyumbani kwa Diamond) anasubiriwa ndege tausi (Zari) aingie na hapa nipo bize na maandalizi ya kumpokea wifi yangu maana siyo kwa kummisi huku. Yaani natamani sana Sikukuu ya Idd tule pilau naye,” alisema. 

0 Comments

Previous Post Next Post