Kisa Mume,Mwanamke Ajifungulia Polisi


Mwanamke mmoja Amina  Rafael Mbunda (26) mkazi wa Kiswanya,kijiji cha Mgudeni,kata ya mwaya,Tarafa ya Mang'ula wilayani kilombero mkoani Morogoro,anadaiwa kujifungua nje ya kituo cha polisi baada ya kutolewa mahabusu alikokuwa akishikiliwa kwa tuhuma zilizomhusu mumewe aliyedaiwa kuhusika na ununuzi wa kitanda cha wizi.

Mwanamke huyo aliyelazwa kituo cha afya mang'ula alikopelekwa na kulazwa baada ya kujifungua,amedai alikamatwa Juni mosi na polisi,Mwenyekiti wa kitongoji na mwanaume mmoja waliofika nyumbani kwake,saa chache baada ya kuondoka mgambo waliokuwa wakimtafuta mumewe kwa tuhuma za ununuzi wa kitanda cha wizi,ambapo akiwa mahabusu licha ya kulalamika kuumwa uchungu,askari wa zamu alimpuuza hadi alipoona amezidiwa na kumtoa nje alipojifungulia kwenye nyasi bila msaada.

Mganga wa kituo cha afya Mang'ula,aliyetajwa kwa jina moja la Msomba ametafutwa kwa njia ya simu ili afafanue kuhusu afya ya mwanamke huyo na kichanga cha kike kilichozaliwa kikiwa na uzito wa kilo 3.5 kwa mujibu wa kadi yake ya kliniki iliyoonesha pia amejifungua kwa msaada wa ndugu,lakini simu yake iliita bila majibu

0 Comments

Previous Post Next Post