Daimond Kumbe Shabiki Mkubwa wa Timu ya Simba? "Siwezi Kujiita Simba Nikashabikia Chui"

Daimond Kumbe Shabiki Mkubwa wa Timu ya Simba? "Siwezi Kujiita Simba Nikashabikia Chui"

Baada ya kuficha kwa muda mrefu kuhusu timu anayoshabikia hapa Bongo, Dimond Platnumz ameamua kuweka wazi.

Akiongea na Wasafi TV usiku wa jana kwenye ugawaji wa tuzo za Mo Simba Award 2018, msanii huyo amesema yeye hawezi kujiita Simba akashabikia Chui.

“Sikuzote unajua siwaambiagi watu mimi ni timu gani, mimi ni Simba. Mimi siwezi kujiita Simba nikashabikia Chui. Mimi ni Simba na Timu yangu ni Simba ndio maana leo nipo hapa,” Diamond.

Hata hivyo hit maker huyo wa Iyena ameshindwa kutaja wachezaji wake wawili ambao anawakubali kwenye timu hiyo kutokana na madai ya kutotaka kuchonganishwa na wachezaji kwa kuwa wote anawakubali. 

0 Comments

Previous Post Next Post