Askofu Afunguka Kuhusu Kifo cha Mapacha Maria na Consolata

Askofu Afunguka Kuhusu Kifo cha Mapacha Maria na Consolata

Askofu Jimbo Katoliki Njombe, Alfred Maluma amesema vifo vya pacha walioungana,  Maria na Consolata Mwakikuti kinapaswa kuenziwa na Watanzania kukumbushana  wajibu wao kwa watu wenye ulemavu.

"Wameacha somo hilo, tuwajali watu wenye ulemavu hilo ndilo somo walilotuachia Maria na Cobsolata," amesema Akofu Maluma leo Jumatano Juni 6, 2018 katika ibada ya kuaga miili ya pacha hao.

Amesema Mungu aliwaumba pacha hao kwa mfano wa sura yake na akawapa uhai kwa kipindi walichokuwa duniani.

Amebainisha kuwa masista wa shirika la Maria Consolata wameonyesha mfano wa kuigwa kwa kuwaleta pacha hao waliofariki dunia katika hospitali ya Mkoa wa Iringa. 

0 Comments

Previous Post Next Post