Aliyejitosa kwa Zari Afunguka ‘Tunajua Huwezi Kurudiana na Diamond’

Aliyejitosa kwa Zari afunguka ‘Tunajua huwezi kurudiana na Diamond’

Msanii wa muziki wa Injili kutoka nchini Kenya, Ringtone Apoko ameonyesha kuchukizwa na tetesi za Zari kurudiana na Diamond.

Utakumbuka hivi karibuni Ringtone alieleza hisia zake kuwa anataka kumuoa Zari, alienda mbali zaidi kwa kueleza kuwa alishanunua gari aina ya Range Rover Sport ya mwaka 2017 kwa ajili ya mrembo huyo.

Soma Pia; Aliyetangaza kumnunulia Zari Range Rover Sport 2017 ala za uso

Sasa Rington Apoko amesema atashangaa ikiwa Zari atarudi kwa Diamond ingawa anajua hawezi kufanya hivyo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;

Mpendwa Zari huwezi ukaendelea kusoma kurasa za kitabu kile kile kila siku ilihali unajua kitakavyoishia, ulioandoka Misri ukaenda Kanani itasikitisha kama utarudi tena.

Nini kitatokea kwa wasichana kibao uliowaambia sasa unamjenga Zari? Ushauri wangu ni kuwa hivi sasa mtafute Mungu kwa kufunga na maombi ili Mwenyezi Mungu akupe mwelekeo. Lakini hivi sasa hatuna wasiwasi maana wote tunajua huwezi kurudiana na Diamond.

Muimbaj huyo amekuwa akituma jumbe mbali mbali kwa Zari kupitia mtandao, hata hivyo Zari akiwa nchini Kenya May mwaka huu alisema hamjui Ringtone kwani ana followers zaidi ya milioni 3.9 katika mtandao wa Instagram. Kumekuwa na taarifa zinazodai kuwa huenda Diamond na Zari wamerudiana au kufanya hivyo hivi karibuni. 

0 Comments

Previous Post Next Post