Zari Asema Hawezi Kumpeleka Diamond mahakamani kwa Sababu ya Matunzo ya Watoto


Mwanamama Zari the Bossy Lady ambae alibahatika kupata watoto wawili na msanii Diamon Platinumz lakini baadae wawili hao walikuja kutengana hivyo Zari kuondoka na watoto na kwenda nao afrika kusini amefunguka na kusema kuwa hata siku moja hawezi na hajawahi kufikiria kwenda kumpeleka mwanaume huyo mahakamani kwa sababu ya matunzo ya watoto.

Akiongea na waandsihi wa habari nchi Kenya, Zari amesema kuwa anatengeneza pesa zake mwenyewe ambazo zinamtosha kwa ajili ya matunzo yake na watoto wake kwahiyo hawezi kuhangaika kumpeleka Diamond mahakamani kwa sababu  hiyo kama wanawake wengine.

Katika historia, Diamond alishawahi kupelekwa mahakamani na Hamisa Mobeto kutokana na kushindwa kutoa matunzo ya mtoto .

Zari ambae ana watoto watano huku watatu wakiwa wa mwanaume mwingine ambae pia alishafariki, amekuwa akionekana kuwalea watoto wake kwa starehe bila shida yoyote kutokana na kusadikika kuwa mwanamke huyo ni tajiri na hana shida ya kuomba misaada. 

0 Comments

Previous Post Next Post