Wema Sepetu Abadili Gia Wasafi TV,Atupilia Mbali Kipindi Chake.


Baada ya Mrembo Wema Sepetu kuweka wazi anakuja na TV Show yake ndani ya Wasafi TV, amefunguka nini hasa kinaendelea kwa sasa.

Kipya cha kufahamu ni kwamba kipindi hicho cha Wema Sepetu hakitakuwa reality show kama ilivyokuwa mwanzoni kikiruka EATV.

“Kitakuwa ni kipindi cha tofauti tutakuwa wanadada watatu. Sitapenda kuweka wazi zaidi lakini haitakuwa reality show, kama itakuwa ni reality show nitaweka kwenye App yangu,” Wema ameiambia Bongo5.

“Bado hatujaanza ku-shoot kwa sababu sasa hivi bado wanafanya majaribio, kwa hiyo ile process nzima ya vipindi bado haijanza, so content zipo pale pale na tutaanza ku-shoot hivi karibuni,” ameongeza.

Utakumbuka hapo awali Wema Sepetu ndiye alikuwa wa kwanza kuweka wazi kuwa Diamond atakuwa Boss wake kupitia Wasafi Tv. 

0 Comments

Previous Post Next Post