Wachungaji Watatu Waliodai Wana Uwezo wa Kufufua Maiti Wanusurika Kichapo.


MPANDA, KATAVI: Wachungaji watatu waliodai wana uwezo wa kufufua marehemu wamenusurika kupigwa na wananchi baada ya kushindwa kumfufua marehemu Raymond Mirambo katika kijiji cha Sitalike

Mwenyekiti wa kijiji, Christopher Angelo, alisema tukio hilo lilitokea Mei 7 ambapo wachungaji hao walifika katika ofisi ya Kijiji na kujitambulisha kuwa wao ni wachungaji kutoka Kijiji cha Nsimbo na wameitwa na ndugu wa marehemu

Baada ya kujitambulisha walienda nyumbani kwa marehemu na kuanza maombi yaliyofanyika kwa muda wa siku 7 usiku na mchana pasipo kuwa na mafanikio yoyote, hali ambayo iliwafanya ndugu wa marehemu washikwe na hasira

Wananchi, ndugu na jamaa walikasirika kutokana na kuona kuwa wachungaji hao wanawatapeli na kwa sababu waliwasababishia kuingia gharama kubwa ya kulisha watu waliokuwa wakishiriki maombi hayo

Angelo anaendelea na kusema baada ya kufika eneo la tukio walikuta vurugu za wananchi wakitaka kuwapiga wachungaji hao, walochokifanya ni kuwaondoa eneo la tukio

0 Comments

Previous Post Next Post