Tunda Man Asaliti Wana...Adai Alikiba Amemzidi Diamond Mbali.

Msanii wa muziki Bongo, Tunda Man amefunguka na kusema kuwa mashabiki wanaowashindanisha Alikiba na Diamond wanakosea.

Muimbaji huyo kupitia Refresh ya Wasafi TV amesema kuwa Alikiba amemzidi Diamond na kinachotakiwa kuwepo kati yao ni heshima tu.

“Hata wale wanaowashindanisha Diamond na Alikiba ni kitu kibaya sana kwa sababu wanachangia vitu vya…, kwa sababu Alikiba ni mkubwa, hiyo ni heshima tu inatakiwa iwepo halafu vitu vingine vinaendelea kama kawaida,” amesema Tunda Man.

Katika hatua nyingine Tunda Man ameeleza kushangazwa na kile alichodai kuwa Diamond anamuona snitch kwa vile yupo karibu na Alikiba.

Tunda Man ameeleza kuwa urafiki wake na Alikiba ulikuwepo toka siku nyingi kabla hata hawajaanza muziki na hata alipowashirikisha wote wawili katika video ya wimbo ‘Starehe Gharama’ Diamond alikuwa anaona urafiki wao.

“Kwenye Starehe Gharama Alikiba amefanya chorus, amefanya intro, Naseeb hajafanya chochote lakini alikuwepo, why sasa hivi ananiona snitch,” amehoji.

“Naseeb ni kama mdogo wangu kwa sababu mimi nimemzidi kwa vitu vingi sana, kwa hiyo kufanikiwa na kutofanikiwa ni mipango ya Mwenyenzi Mungu lakini heshima ni kitu kikubwa sana katika maisha,” amesema.

Tunda Man kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya’ Boss Hanuniwi’, ambavyo ilitoka pamoja na ngoma nyingine mbili.

0 Comments

Previous Post Next Post