Tunda Man amchana Bob Junior.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Tunda Man ambaye hivi karibuni ameachia kazi mpya, amempa makavu Bob Junior baada ya kusema kuwa amekurupuka kuachia kazi zaidi ya moja kwa pamoja, na kumtaka amuheshimu.
Akizungumza na eNewz ya East Africa Television, Tunda Man amesema kwamba Bob Junior ni mdogo kwake kimuziki na kila kitu, hivyo hawezi kumsh\uri kitu kwenye muziki wake, hivyo hesima lazima ichukue mkondo wake baina yao.
“Mimi na Bob Junior ni vitu viwili tofauti, mimi nimeanza muziki muda mrefu yeye ameanza juzi juzi tu hapa, mimi kwenye muziki Bob Junior hawezi kunishauri kitu kikaendanana na muziki wangu, yeye naimbie tu ngoma umetoa kali, kitu kikubwa mimi na Bob Junior tuko tofauti kabisa, mimi mkubwa kwake kiumri, mkubwa kwake kimuziki, lazima heshima ifuate mkondo”, amesema Tunda Man.
Sambamba na hilo Tunda Man amesema ataendelea kuachia kazi mpya ndani ya wiki hiii, kwani kitu kilichokuwa kikimzuia kimeshaisha, hivyo mashabiki wake wajiandae kupata burudani kutoka kwake.

0 Comments

Previous Post Next Post