Toka Nijue Mapenzi Sijawahi Kuiba Mume wa Mtu-Thea.

Toka Nijue Mapenzi Sijawahi Kuiba Mume wa Mtu- Thea

WAKATI mastaa wengi wa kike Bongo wakizungukana na kuchukuliana mabwana, mkongwe wa maigizo Bongo, Salome Urassa ‘Thea’ amevunja ukimya kuwa, tangu ajue mapenzi ni kitu gani, hajawahi kuiba mwanaume wa mwanamke mwenzake.Akizungumza na Za Motomoto News, Thea alifunguka kuwa, suala la kuibiana mabwana halipo kwa wasanii tu, bali ni kwa jamii nzima, lakini kwa upande wake hajawahi  kumzunguka mtu kwa kuwa hiyo ni tabia ya mtu na kwake haipo.“Kiukweli tangu niyajue mapenzi, sijawahi kuiba bwana wa mtu kwa sababu siyo tabia yangu na siwezi kufanya hivyo, wanaochukua mabwana za watu ni tabia zao ambazo huwezi kuzibadilisha na hii haipo kwa wasanii tu, bali ni kwa jamii kwa jumla kwani tumekuwa tukisikia sana ila kwa wasanii wanaonekana zaidi kutokana na majina waliyonayo,” alisema Thea.

0 Comments

Previous Post Next Post