TFF Yapangua Ratiba ya Ligi Kuu.

TFF Yapangua Ratiba ya Ligi Kuu

Shirikisho la soka nchini kupitia kwa Bodi ya ligi (TPLB), limepangua mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara kati ya Mbao FC na Ndanda FC uliokuwa unatarajiwa kucheza Ijumaa ijayo.

Taarifa ya TFF leo, imeeleza kuwa mchezo huo umerudishwa nyuma kwa siku moja ambapo badala ya kuchezwa Ijumaa sasa utachezwa Alhamisi ya wiki hii sababu kubwa ikiwa ni uwanja kuwa na shughuli nyingine.

''Mchezo wa Ligi Kuu kati ya Mbao FC ya Mwanza na Ndanda FC ya Mtwara uliokua uchezwe Mei 11, 2018 umerudishwa nyuma utachezwa Mei 10, 2018 Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, kufuatia Uwanja huo kuwa na matumizi mengine ya kijamii'', imeeleza taarifa hiyo.

Mbao FC inashika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi kuu kwenye mechi 26 ilizocheza huku ikiendelea kuwa kwenye mstari wa kushuka daraja. Ndanda nayo ipo nafasi ya 15 ikiwa na alama 22 baada ya mechi 27.

0 Comments

Previous Post Next Post