TANZIA: Aliyekuwa Kocha wa Yanga Afariki Dunia.

Aliyekuwa Kocha wa Yanga Afariki Dunia

Aliyekuwa Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Jack Chamangwana amefariki dunia hapo jana siku ya Jumapili majira ya jioni kwenye Hospitali ya Queen Elizabeth (QECH) nchini Malawi.

Ripoti zinaeleza kuwa chanzo cha kifo chake ni kutokana na shinikizo la Moyo hii ikiwa ni Mwezi mmoja umepita toka kumzika mpwa wake, George Chamangwana.

Wakati wa uhai wake Chamangwana maarufu kwajina la ‘Africa’ alikuwa Mkurugenzi wa ufundi ndani ya klabu ya Be Forward Wanderers ya nchini Malawi.

Nahodha huyo wazamani aliyekuwa na umri wa miaka 61, aliwahi kuifundisha timu ya Yanga mwaka 2006 kabla kutimka zake kwao.

Chamangwana ameanza kuitumikia timu yake ya Taifa ya Malawi kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Kenya Julai 10 mwaka 1975 akiwa na umri wa miaka 18 huku goli lake la kwanza akifunga dhidi ya Botswana.

0 Comments

Previous Post Next Post