Tanzania Hatuna Bahati Kwenye Mpira..Ngorongoro Heroes yafungashiwa vilago U20.


Vijana wa timu ya taifa chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes wametupwa pembeni ya mbio za kuwania tiketi za Fainali za U20 Afrika baada ya kuchapwa mabao 4-1 na wenyeji, Mali kwenye Uwanja wa Omnisports Modibo Keita mjini Bamako.


Matokeo hayo yanamaanisha Tanzania inatolewa katika mchakato wa kuwania tiketi ya Niger mwakani kwa jumla ya mabao 6-2, baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kwenye mchezo wa kwanza Mei 13 Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.

Vilevile katika mchezo wa kwanza Kabwili hakuweza kucheza baada ya kutopangwa na Kocha Mkuu Ammy Ninje lakini alianza katika kikosi cha leo.

Mali sasa itakutana na mshindi wa jumla kati ya Cameroon na Uganda katika hatua ya mwisho ya mchujo kuelekea Niger 2019.

0 Comments

Previous Post Next Post