TAARIFA KUTOKA IKULU JUU YA RAIS MAGUFULI NA MECHI YA SIMBA SC


Leo May 19, 2018  Imethibitishwa kuwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli atashiriki katika zoezi la kupokea Kombe la Ubingwa wa CECAFA pamoja na kuwakabidhi kombe la mabingwa wa michuano ya ligi kuu soka Tanzania Bara mabingwa wapya Simba SC.

Kupitia ukurasa wa Twitter wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais- Ikulu, Gerson Msigwa amesema Rais Magufuli ataungana na wanamichezo katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
“Rais  Magufuli leo ataungana na wanamichezo kupokea kombe la ubingwa wa CECAFA kutoka timu ya Serengeti Boys, kuipokea timu ya TSC iliyoibuka mabingwa wa pili wa dunia huko Urusi na kukabidhi kombe kwa Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 8 mchana” amesandika Msigwa.

Tukio hili la kimichezo ni kwa Rais Dkt. Magufuli ndio la kwanza kulifanya tokea alipoingia madarakani na hivyo atakuwa amewawekea historia kubwa klabu ya Simba SC kukabidhiwa kikombe na Rais pamoja na Serengeti Boys.

0 Comments

Previous Post Next Post