Sugu Mzuri, Niko Tayari Kumpa Tena- Faiza Ally


Faiza Ally ambaye ni muigizaji wa Bongo movie na mama watoto wa Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi 'Sugu’ amesema kuwa hayuko tayari kuolewa na mzazi mwenzake huyo bali anaweza mzalia mtoto mwingine.


Faiza amefunga hayo katika mazungumzo yake na eatv.tv ambapo amesema kuwa hana ndoto za kuolewa na Sugu bali anaweza mpatia mtoto mwingine kwakuwa ana mbegu nzuri na kujivunia kuwa binti yake ni mzuri kama baba yake.

“Sugu naweza mzalia mtoto mwingine maana ana mbegu nzuri kanipatia mtoto mzuri sana lakini sio kuolewa nae maana tulishindwana awali sidhani kama tunawezana tena”, amesema Faiza.

Mwana dada huyo mwenye watoto wawili hivi sasa ameendelea kusema kuwa ataongeza mtoto mwingine endapo atapata kipato zaidi lakini kwa sasa hali yake inamruhusu watoto wake hao wawili. 

0 Comments

Previous Post Next Post