Skendo ya Kumtelekeza Mtoto, Mbasha Yamkuta ya Ali Kiba.


DAR ES SALAAM: Mambo ni hivi! Achana na staa wa Bongo Fleva, Ally Salehe Kiba ‘Alikiba’ kuburuzwa mahakamani kwa kushindwa kutoa matunzo ya mtoto, mwimbaji wa Injili, Emmanuel Mbasha naye amekutwa na skendo kama hiyo baada ya kudaiwa kumtelekeza mwanaye mwenye umri wa miaka mitatu, Risasi Mchanganyiko linakuwa la kwanza kukuletea mkanda kamili.

 Chanzo makini kililieleza Risasi Mchanganyiko kwamba, hivi karibuni Mbasha aliburuzwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar na mama mtoto wake ambaye ni mjasiriamali anayejulikana kwa jina la Miriam Kawishe. Miriam alimlalamkia Mbasha kumtelekezea mtoto huyo waliyezaa pamoja aitwate Avantica kwa kutompa matunzo tangu azaliwe hadi hivi sasa ambapo ana umri wa miaka mitatu.

 “Unajua Mbasha naye ameburuzwa mahakamani kwa kesi ya kushindwa kutoa matunzo ya mtoto tangu alipozaliwa hadi sasa ana miaka mitatu na ilianza kutajwa wiki iliyopita huku ikitarajiwa kuendelea tena mwisho wa mwezi huu.“Ninyi mtafuteni huyo mzazi mwenzake atawaeleza vizuri,” kilisema chanzo hicho.

 Baada ya kupata habari hiyo, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta mwanamama huyo aliyezaa na Mbasha, Miriam ambaye alikiri kwamba ni kweli, lakini hawezi kuzungumza sana kwani kwa sasa suala hilo liko mahakamani tayari pia ana wakili anayelisimamia.

 Wimbi la mastaa kudaiwa kutelekeza watoto na kushindwa kuwapatia matunzo limeendelea kuzidi kila kukicha ambapo lilianza kwa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kukataa kutoa matunzo kwa mtoto aliyezaa na mwanamitindo Hamisa Mobetto na kupelekeshana mahakamani.

Hivi karibuni Alikiba naye aliburuzwa mahakamani kwa skendo kama hiyo na mpaka sasa kesi yake inaendelea.

STORI: Mwandishi Wetu, Risasi Mchanganyiko 

0 Comments

Previous Post Next Post