Sir Alex Ferguson afanyiwa upasuaji kwenye ubongo.

Kocha wa zamani wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson jana Mei 05, 2018 amefanyiwa upasuaji mdogo kwenye kichwa.
Sir Alex Ferguson
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ukurasa rasmi wa Twitter wa klabu ya Manchester United, imeelezwa kuwa upasuaji huo unahusisha ubongo na umeenda salama.
Hata hivyo, hakuna taarifa rasmi kuhusu tatizo linalomsumbua Mzee Ferguson hadi kufanyiwa upasuaji huo.
Kufuatia hali hiyo, Mtoto wa Sir Alex aitwaye Darren Ferguson ambaye pia ni kocha wa klabu ya Doncaster jana alishindwa kuhudhuria mechi kati ya kalbu yake dhidi ya Wigan.
Hata hivyo, baadhi ya wachezaji wametoa pole kwa mzee Ferguson kufuatia taarifa akiwemo Robin Van Persie, Pepe Reina, Diego Forlan, Bacary Sagna na wengineo.
Pole nyingine zimetoka kwa vilabu vikubwa kama Barcelona, AS Roma, Chelsea, Manchester City, Arsenal na vilabu vingine vikubwa.

0 Comments

Previous Post Next Post