Sijui Kilichonifanya Niachiwe Kwani Nilijua Nitaachiwa Huru Mwezi wa 6- Mbunge Sugu.

Sijui Kilichonifanya Niachiwe Kwani Nilijua Nitaachiwa Huru Mwezi wa 6- Mbunge Sugu

Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu ambaye ameachiwa huru leo kutoka gerezani alikofungwa akiwa na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga, amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya kutoka jela.


Akizungumza na East Africa Radio, Sugu amesema hakuwa anajua kama anaachiwa mpaka pale alipofuatwa na polisi kuambiwa ajiandae, na hajui imekuwaje mpaka akaachiwa sasa kwani ilijulikana ataachiwa huru mwezi wa 6.

“Watu wote walikuwa wanatarajia nitoke mwezi wa 6, lakini ghafla hapo jana niliambiwa nijiandae kwamba kesho asubuhi natakiwa niachiwe, kutoka nje nikakuta askari wengi na nikaelekezwa kuingia kwenye gari la RCO mimin a mwenzangu Masonga, tukasindikizwa na maafisa magereza watano wakatupeleka mpaka nyumbani na kutukabidhi kwa familia”, amesema Sugu.

Sugu ameendelea kusema kwamba..."watu wanauliza imekuwaje lakini mimi nawaambia sijui kwa sababu haikuwa kazi yangu kufanya hesabu za magereza, hiyo ni kazi ya magereza, kwa sababu mimi kama mimi ninachoamini sikutakiwa kuwa magereza in the first place, utumishi uko pale pale kwa level ile ile tulikuwa na exposure sasa hivi tumeongeza experience”.

Wawili hao wameachiwa huru leo kutoka gereza kuu la Ruanda mkoani Mbeya walikokuwa akitumikia kifungo chao cha miezi mitano, jambo ambalo limewashtua wengi kwani inaaminiwa muda wake ulikuwa bado haujaisha.

0 Comments

Previous Post Next Post