Shilole Ajipanga Kurudi shule Kuongeza Maarifa.

Shilole Ajipanga Kurudi shule Kuongeza Maarifa

Baada ya siku chache zilizopita mrembo na mjasiriamali, Zewena Yusuf Mohammed aka Shilole kutembelea chuo cha National College of Tourism NCT kwaajili ya kujionea kozi mbalimbali zinazotolewa chuoni hapo, mrembo huyo ameahidi kurudi chuoni hapo kwaajili ya kuchukua kozi ya mafunzo ya upishi.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chuo hizo, zinadai muimbaji huyo alivyotembelea chuoni hapo mapewa wiki iliyopita, aliahidi kurudi kuchuoni hapo pamoja na team yake kwaajili ya kuchukua kozi ya mapishi.


“Siri ilifichuliwa🔓na mwanamuziki🎼 Shilole @shilolekiuno_badgirlshishi mmiliki wa mgahawa wa Shishi food👨‍🍳Kumbe mambo yanalipa ila na yeye hakusita kufika NCT kuweza kuiongeza thamaniđź’Ž yake na biashara yake ya chakula kwa kupata Dondoo juu ya Ukarimu na ufahamu katika maswala ya ujasiriamali kisha utaalamu wa juu katika FOOD PRODUCTION🍛🥪 Alichosema atakuja yeye na timu yake kupata kozi fupi. Ulikuwa wakati mzuri kukutana na anayeitumikia sekta ya ukarimu na wale wanaojiandaa kuingia. Fursa bado ni nyingi. Hataki ujinga wa kupishana na fursa we unasubiri nini. Ahsante🙏🏽 @shilolekiuno_badgirlshishi kwa kupata nafasi ya kututembelea na karibu sana NCT. Kwa maelezo juu ya kozi zinazotolewa tembelea website yetu link IPO kwenye bio.. #shishifood #Daresalaam #utalii #ukarimu#nctaladdertoexcelence,”

Mrembo huyo ambaye ni mke wa Uchebe, ana miaka miwili kwa sasa anaendesha biashara ya mgahawa.

0 Comments

Previous Post Next Post