Samatta Awaonya Serengeti Boys " Tulizeni Vichwa Madogo Tusije Kusikia Mmeanza Kuoa"

Nahodha wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars Mbwana Ally Samatta amewapongeza vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kwa kutwaa ubingwa wa CECAFA Challenge U-17 nchini Burundi.


Serengeti Boys Jumapili ilifanikitwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Challenge U-17) kwa kuwafunga vijana wa Somalia, mabao 2-0 yaliyofungwa na Edson Jeremiah dakika ya 25 na Jaffar Mtoo dakika ya 66.

“Hongereni sana 'Serengeti' (U17) kwa ubingwa wa CECAFA kwa umri wa chini ya miaka 17. Tunaamini TFF ina mipango mikubwa juu yenu. Tulizeni vichwa madogo, tusianze kusikia mmeanza kuoa sasa (utani). Hongereni sana,”. Samatta ameandika kupitia 'Twitter'.Serengeti Boys imerejea nchini Alfajiri ya leo na kupokewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe ambaye amewapongeza vijana kwa ushindi huo.

0 Comments

Previous Post Next Post