Sallam SK alisaini kundi la Nany Kenzo, Diamond kuiachia video ya wimbo Baila.

Meneja wa Diamond na AY, Sallam SK jana katika sherehe ya siku yake ya kuzaliwa ametangaza kulisimamia Kundi la Muziki la Nanvy Kenzo.

Sallam amesema kuanzia wiki ijayo kazi za kundi hilo ambao lilikuwa kimya zitaanza kuachiwa.

“Exclusive mimi ni meneja wa Nany Kenzo, nimeshawasaini na kuanzia wiki ijayo naanza nao kazi,” alisema Sallam kupitia Dizzim Online. “Kwahiyo Aika na Nahreel wapo chini ya SK kibiashara kuanzia sasa hivi,”

Aliongeza, “Naomba niongezee video ya Diamond Platnumz Baila inatoka hivi karibuni, halafu AY ana project kama tatu na mpaka sasa hivi hatujajua ipi itoke lakini nadhani leo tulikuwa tunampango wa kupiga ana anadoo. Kwa upande wa Nany Kenzo wana project tano wameshoot video zote, kwa hasira wamesema ukiwa kama meneja wetu mpya tunakuletea video 5 chagua yoyote ambayo inatoka kwahiyo ni mtihani mgumu, kwahiyo katika video itayotoka ya Navy Kenzo nitaichagua mimi, kama nitakuwa nimekoseha nisameheni,”

Nao Nany Kenzo amethitisha kusainiwa na Sallam SK huku wakiwaahidi mashabiki wao kazi nyingi hivi karibuni. 

0 Comments

Previous Post Next Post