Qeen Darleen Ampa Ujumbe Mzito Harmonize "Punguza Uhuni Unamtesa Mzungu wa Watu"


First Lady kutoka Label ya WCB, Queen Darleen ametoa ushauri mzito kwa Harmonize kuhusu maisha yake ya kimuziki na mahusiano.

Muimbaji huyo amemshari Harmonize kutokata tamaa na muziki wake ingawa watu wa kumkatisha tamaa wapo, huku akimsisitiza kuwa kuepeka kuwa katika mahusiano na wanawake wengi.

“Apunguze uhuni, atulie, mtoto wa watu masikini ya Mungu, Mzungu (Sarah) anampenda, yeye muhuni. Mdogo wangu maisha ya uhuni siyo mazuri, unakuwa kama mfalme Sulemani, ache hizo,” Queen Darleen ameiambia Radio Five.

Harmonize na Queen Darleen wameshakutana katika ngoma inayokwenda kwa jina la Zilipendwa ambayo ilikutanisha wasanii kama Diamond, Lava Lava, Rayvanny, Rich Mavoko na Mbosso. 

0 Comments

Previous Post Next Post