Producer wa Mariah Carey,Michael Jackson afanya kazi na Vanessa Mdee(@VanessaMdee).Vanessa Mdee amekuwa akipambana kwa kila hali kuhakikisha muziki wake unafika mbali zaidi. Msanii huyo amekutana na producer na audio engineer, Humberto Gatica ambaye ni mshindi wa tuzo 16 za Grammy na kufanya naye kazi.

Vanessa amekutana na producer huyo katika studio maarufu duniani ya Abbey Road iliyopo nchini Uingereza na kutengeneza project ya kazi kwa ajili ya tamasha la Bantu Jazz litakalofanyika Juni 9 ya mwaka huu nchini Garbon.

Akiongea na mtangazaji Fredrick Bundala, Vee Money amesema kuwa Gatica pia atakuwepo kwenye tamasha hilo litakalofanyika Garbon.

Gatica amewahi kufanya kazi na wasanii wakubwa duniani akiwemo Barbra Streisand, Mariah Carey lakini kubwa zaidi ni Thriller ya Michael Jackson, My Heart Will Go On ya Celine Dion na nyingine.

0 Comments

Previous Post Next Post