Penzi la Davido,Chioma Lazidi Kushika Kasi ni Bata tu.

Penzi la David, Chioma  Lazidi Kushika Kasi

Msanii Davido na mpenzi wake Chioma wamezidi kuonyesha mapenzi yao ni kama njiwa baada ya kuyafanya siri kwa muda mrefu.

Davido ameweka picha kwenye mtandao wake wa Instagram akiwa na mrembo wake huyo huku wakionekana wenye furaha kubwa na kuandika kwenye moja yapicha ujumbe unaosomeka, “Happy people 😁.”

Msanii huyo wiki iliyopita alimzawadia mrembo wake huyo gari aina ya Porsche SUV yenye thamani ya kiasi cha dola 125k ambapo ni zaidi ya shilingi milioni 285 za Kitanzania kwenye birthday yake.

0 Comments

Previous Post Next Post