Ng’ombe waliokufa wakamatwa wakiingizwa Sokoni.


Mapema asubuhi ya leo katika Machinjio ya Tegeta lilikamatwa lori lililopakia ng’ombe waliokufa wakiwa tayari kuingizwa sokoni.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, ACP Jumanne Muliro amesema kuwa kufariki kwa mifugo ni tukio la kawaida kwani Mifugo inatoka mbali na ikitokea hivyo kuna utaratibu unaotakiwa kufanyika na si kuwaingiza sokoni mifugo hao.

“Malori yanasafiri na mifugo umbali mrefu na mifugo mingine hufariki kutokana na hali hiyo na tayari maafisa mifugo walifika katika eneo la tukio na kuhakikisha wanashughulikia tatizo hilo mapema”. Amesema Kamanda Murilo

Kamanda Muliro ameongeza kuwa Sheria na kanuni zinaeleza endapo likitokea tukio kama hilo nini kifanyike ili kulinda Afya za walaji.

0 Comments

Previous Post Next Post