Ndugu wa Masogange hawajapewa michango ya marehemu.

Ndugu wa marehemu Masogange wakiwemo wifi zake ambao pia ndio wanaishi na mtoto wake Sania, wamesema hawajapata taarifa zozote juu ya pesa ambazo zilichangwa na kamati ya wasanii, kwa ajili ya kumsaidia mtoto.
Wakizungumza na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, mmoja wa ndugu hao aliyejulikana kwa jina la Sada, amesema hawajapata taarifa yoyote kutoka kwa kamati hiyo iliyoundwa na wasanii, ambayo pia ilisimamia kwa kiasi kikubwa mazishi ya Agnes Masogange, na wala hawajawasiliana nao.
“Toka tumekuja hatujapata taarifa zozote, bado hatujawasiliana nao mpaka dakika hii, labda mpaka tuwatafute”, amesema Sania.
Sambamba na hilo ndugu hao wamesema wao wenyewe kama familia wamejipanga kumlea mtoto huyo kwani walikuwa wanamlea hata wakati wa uhai wa mama yake Agnes Masogange.
Baada ya Agness Masogange kufariki kamati maalum iliyoundwa na wasanii mbali mbali wa bongo movie na filamu, walichangisha pesa kwa ajili ya kumsaidia mtoto wa marehemu Sania, ili iweze kumsaidia atakapoingia kidato cha kwanza.

0 Comments

Previous Post Next Post