"Naogopa Kufilisika Ndio Maana Sitoi Nyimbo Mara Kwa Mara" - Alikiba


Msanii wa Muziki wa kizazi kipya anayefanya vizuri kwa sasa na ngoma yake ya 'Mvumo wa radi', Alikiba amesema ana uwezo wa kutoa nyimbo kila siku lakini anaogopa kufirisika.


Kiba amesema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio ambapo amesema kuwa anauwezo wa kutoa nyimbo kila siku lakini anahofia kufirisika kwakuwa muziki unatumia pesa.

“Sio kama siwezi kuachia ngoma mfululizo naweza achia ngoma mwezi mzima yaani kila siku lakini naogopa kufirisika muziki unatumia pesa nyingi”. Amesema Kiba

Kiba ameongeza kuwa pia kukaa kutoa wimbo na kuupa muda mashabiki wanakuwa wanamuona mpya kwani kutoa kila siku unaweza chokwa mapema. 

0 Comments

Previous Post Next Post