Nandy Afunguka Kuhongwa Gari la Mamilioni.

SIKU chache baada ya kusambaa mitandaoni kwa picha zake zikimuonesha akiwa na gari jeusi la mamilioni aina ya Mercedes Benz E-Class E320 CDI, msanii wa Bongo Fleva, Faustina Charles ‘Nandy’, amefungukia ndoa yake ijayo na gari hilo kuwa amelinunua kwa jasho lake na hajahongwa na mtu kama watu wanavyoeneza.

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Nandy alisema kuwa, gari hilo alilinunua kwa zaidi ya shilingi milioni 70 za Kitanzania kwa jasho lake na hiyo ilitokana na kuingia mikataba na makampuni mbalimbali Tanzania yakiwemo ya michezo ya namba, shirika moja kubwa la ndege na mingineyo.

“Watu wengi wanajua kuwa kuna mtu ameninunulia hili gari, lakini siyo kweli kabisa, mimi mwenyewe nina madili mengi ya kufanya na ndiyo yameniwezesha kupata fedha za kununua Benz, yaani kifupi ni jasho langu mwenyewe,” alisema Nandy.


Nandy pia aliongeza kuwa, kwa sasa amekuwa na amani baada ya kupitia kipindi kigumu.

“Unajua nimepita katika wakati mgumu sana, lakini sikumuacha Mungu kabisa na ndiyo maana hata haya yote yanayonitokea ya kupata mikataba na kufanikiwa hadi kununua gari ni kwa sababu kila kitu changu sasa kiko sawa kabisa,” alisema.

Kabla ya gari hilo, Nandy alikuwa akitumia gari aina ya Toyota Harrier. Hivi karibuni aliingia kwenye kashfa baada ya video yake ya faragha kuvuja akiwa na Bill Nas na kusambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, jambo ambalo lilimpa fedheha kubwa.


Kuhusu mipango ya ndoa, Nandy alisema kuwa, kuna mipango kabambe ambapo ataolewa hivi karibuni huku akigoma kumwanika mchumba’ke akihofia nyakunyaku wa mjini.

“Nimewaambia tu ninyi kwa sababu mmeniwahi kuniuliza, ukweli ni kwamba nitafunga ndoa soon, lakini kuhusu mwanaume wangu, naomba nisimwanike kwa sasa,” alisema Nandy.

0 Comments

Previous Post Next Post