Mwanamuziki Justin Bieber Amrudia Mungu.
NYOTA wa muziki wa pop nchini Marekani, Justin Bieber, ameanza kurudi kanisani baada ya aliyekuwa mpenzi wake, Selena Gomez, kutumia ukurasa wake wa Instagram na kusema ‘hawezi kurudi nyuma’.

Kauli hiyo ya Selena imekuja mara baada ya kutangaza kuwa anatarajia kuachia wimbo wake mpya hivi karibuni.

Aliyekuwa mpenzi wa staa wa pop, Justin Bieber, Selena Gomez, amezidi kumchanganya staa huyo baada ya kutumia ukurasa wake wa Instagram na kutangaza kuwa anataka kuachia wimbo wake mpya ujulikanao kwa jina la ‘Back 2 You’, hivyo mashabiki waliamini kuwa wimbo huo unamaanisha anataka kurudi kwa mpenzi wake huyo wa zamani baada ya kuachana.

Mrembo huyo aliamua kuwajibu mashabiki hao kwa kusema hawezi kurudi nyuma kama wanavyodhani, hivyo kauli hiyo imemfanya Bieber kuanza kurudi kanisani kwa ajili ya kumwomba Mungu.

Siku za hivi karibuni msanii huyo hakuwa anaonekana kanisani, lakini baada ya kauli hiyo, Bieber ameamua kuanza tena kumkumbuka Mungu. 

0 Comments

Previous Post Next Post