Mtoto wa Masogange akataa shule hizi.


Mtoto wa video queen maarufu bongo Agnes Masogange ambaye alifariki mwishoni mwa mwezi uliopita,Sania Shaaban, amekataa kusoma shule za bweni ambazo ameahidiwa kusomeshwa na wafadhili, na kutaka kusoma shule za kutwa.

Akizungumza na Big Chawa kwenye Planet3 Bogno ya East Africa Radio, Sania amesema hataki kukaa mbali na shangazi zake ambao ndio wanamlea, na hajazoea shule hizo.

“Napenda kukaa nyumbani kwa sababu nitawamisi shangazi zangu, shangazi zangu wote nawapenda na sijawahi kukaa mbali nao”, amesema Sania.

Kwa upande wa shangazi zake ambo wanamlea Sada na Samia wamesema mtoto huyo hajawahi kukaa mbali na wao, hivyo suala la kwenda kusoma shule za bweni itabidi lifikiriwe kwanza kwa ajili ya usalama wake.

0 Comments

Previous Post Next Post