Mrisho Mpoto Ft Harmonize | Mpoto amuweka Harmonize kwenye ngoma yake mpya.

Uliwahi kufikiria kama unaweza ukamuona msanii kama Harmonize kwenye ngoma ya Mrisho Mpoto?
Basi wawili hao tayari wameshapika ngoma ambayo inaweza ikasikika kwenye masikio yako muda wowote.
Tena wimbo huo unaonekana kupewa jina la Mjomba kutokana na ujumbe ambao ameuandika Harmonize kwenye mtandao wa Instagram akimshukuru Mpoto kwa kumuweka kwenye wimbo huo ambapo ilikuwa ni ndoto zake za siku nyingi kufanya kazi na mkali huyo wa kuandika mashahiri yenye ujumbe na mafumbo mazito.
Kupitia mtandao huo, Harmo ameandika:
Binafsi nikiionaga sura yako naona inaashiria Amani, Upendo, Furaha, Hekima, na Busara….!!! Naamini tupo wengi sana…!!! wenye mtazamo kama wangu wewe ni kama Nembo ya Tanzania kwani hata viongozi hujivunia uwepo wako katika Sanaa nichukue fursa hii kusema Asante sana….!!! Kwa kuniamini na kunipa nafasi ya kushiriki katika kazi yako #Mjomba @mrishompoto M/mungu akubariki sana….!!! hii nikama ndoto kwangu đź™Źđź™Ź kama wewe ni mzalendo na unamkubali #Mjomba comment #Yess

0 Comments

Previous Post Next Post