Mnyika na Bulaya Watolewa Bungeni.


Naibu Spika Tulia Ackson ameagiza Mbunge wa Kibamba Mhe. John Mnyika na Ester Bulaya kutolewa nje ya ukumbi wa Bunge kwa kile alichodai kutoheshimu kiti cha Spika.

Naibu Spika ametoa maamuzi hayo jioni ya leo Mei 9, 2018 katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji mwaka 2018/19 ambapo Mbunge John Mnyika alisimama akitumia kanuni ya 69(1), kutaka kuahirishwa kuhitimishwa kwa hoja ya wizara ya Maji na Umwagiliaji ili apewe nafasi ya kutoa hoja yake ya kwanini bajeti ya wizara hiyo isipitishwe na Bunge.

Mara baada ya kauli hiyo, Dk Tulia alisimama akitumia kanuni ya 69(2), kusema kama Spika atakuwa na maoni kwamba kuwasilishwa kwa hoja hiyo ni kinyume cha uendeshaji bora wa shughuli za Bunge, atakataa kuitoa ili ijadiliwe.

Mbali na Mnyika Naibu Spika Dk. Tulia Ackson amemtoa pia ndani ya Ukumbi wa Bunge, Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya (Chadema) kwa kutoheshimu kiti cha Spika.

0 Comments

Previous Post Next Post