Mlinda Mlango wa Azam Anyakua Tuzo ya Mchezaji Bora Mlinda mlango wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Mwadini Ally amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa timu hiyo mwezi Machi baada ya kupata kura nyingi zaidi alizopigiwa na mashabiki wa timu hiyo. Mwadini ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwa na kiwango kizuri mwezi huo akicheza jumla ya mechi nne sawa na dakika 360 huku akiruhusu wavu wake kutikiswa mara moja tu. Kipa huyo amevuna asilimia 52 za kura 1,000 zilizopigwa na mashabiki wa soka kupitia ukurasa maalum wa kijamii wa Azam FC, kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ amevuna asilimia 25 huku Frank Domayo ‘Chumvi’ naye akivuna asilimia 23 ya kura hizo.

Mlinda Mlango wa Azam Anyakua Tuzo ya Mchezaji Bora

Mlinda mlango wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Mwadini Ally amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa timu hiyo mwezi Machi baada ya kupata kura nyingi zaidi alizopigiwa na mashabiki wa timu hiyo.


Mwadini ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwa na kiwango kizuri mwezi huo akicheza jumla ya mechi nne sawa na dakika 360 huku akiruhusu wavu wake kutikiswa mara moja tu.

Kipa huyo amevuna asilimia 52 za kura 1,000 zilizopigwa na mashabiki wa soka kupitia ukurasa maalum wa kijamii wa Azam FC, kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ amevuna asilimia 25 huku Frank Domayo ‘Chumvi’ naye akivuna asilimia 23 ya kura hizo.

0 Comments

Previous Post Next Post