Mkutano Mkuu wa Dharura Waitishwa Simba Mo Dewji Kukabidhiwa Timu?.

Baada ya Simba kufanya mkutano wa kubariki mabadiliko ya mfumo Desemba 11, 2016 na wanachama kukubali,  Desemba 3, 2017 pia wanachama kwa pamoja walimpitisha Mfanyabiashara Mo Dewji kwaajili ya kuwekeza klabuni hapo na sasa wanaelekea kumkabidhi timu.


Hatua hiyo imekuja baada ya klabu hiyo kuitisha mkutano wa wanachama utakaopitisha Katiba mpya ambayo itatoa baraka rasmi za mfumo mpya wa Hisa kuanza kutumika kuendesha timu.

''Uongozi wa klabu ya Simba unapenda kuwataarifu kwamba kutakuwa na mkutano wa mabadiliko ya Katiba utakaofanyika siku ya Jumapili tarehe 20/05/2018,'' imeeleza sehemu ya taarifa ya klabu.

Katika mfumo huo wa hisa wanachama ndio watakuwa wamiliki wa hisa nyingi wakiwa na asilimia 51, huku mwekezaji akimiliki kwa asilimia 49. Tayari Mo Dewji ameshaweka wazi uwekezaji wake utakuwa na thamani ya bilioni 20.

Baada ya kutangazwa kuwa ndiye mshindi wa zabuni ya kuwekeza, Mo Dewji alieleza vipaumbele vyake kuwa ni kuwekeza kwenye timu za vijana pamoja na miundombinu ikiwemo mabweni ya timu pamoja na uwanja.

0 Comments

Previous Post Next Post