Mbunge Sugu Aachiwa Huru Atoka Gerezani.

Breaking News: Mbunge Sugu Aachiwa Huru Atoka Gerezani

Mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chadema, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ameachiwa huru kutoka gereza la Ruanda, Mbeya alipokuwa akitumikia kifungo cha miezi mitano.

Sugu ameachia huru pamoja na katibu wa Chadema kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, mbunge wa Viti Maalumu, Sophia Mwakagenda na viongozi wengine wa chama hicho walifika gerezani hapo kuwapokea na tayari wamefika nyumbani kwa Sugu.

Wengine waliofika gerezani ni Meya wa Jiji la Mbeya, Mchungaji David Mwashilindi na madiwani.

Sugu na Masonga walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela February 26, 2018 kwa kutoa lugha ya fedhea dhidi ya Rais John Magufuli kwenye mkutano wa hadhara walioufanya Desember 30, 2017 katika uwanja wa shule ya msingi Mwenge, Mbeya. 

0 Comments

Previous Post Next Post