Mambo ni Hivi Mke wa P Funk Agoma Kumuachia Nyumba Kajala "Nitapambana Hadi Kieleweke"


Mke wa Prodyuza maarufu na mkongwe kwenye mziki wa Bongo fleva P Funk majani, Samira ameibuka na kudai atapambana na Kajala na kamwe hatamuachia nyumba.

Kwa Miezi kadhaa Kumekuwa na tetesi kuwa PFunk na Ex wake ambaye pia ni mama watoto wake aliyezaa naye mtoto mmoja Kajala wamerudiana kitu kinachomuweka Pabaya mke wa Pfunk ambaye hivi sasa ni mjamzito.

Samira ambaye wiki iliyopita ilisemekana alikuwa tayari kumuacha Pfunk na kurudi kwa wazazi wake Arusha, inadaiwa ameamua kupambana na Kajala na kukataa kumuacha Kajala amchukue mumewe.

Kwenye mahojiano na GPL, Samira ameongea kwa uchungu huku akidai kila siku huwa anaumizwa pale anapokutana na kashfa kumuhusu mume wake na Kajala lakini ameamua kubaaki kupambana.

"Yaani mateso ninayokutana nayo kwenye ndoa yangu ni Mungu pekee ndio anajua tena kwenye hali hii ya ujauzito niliyo nayo, awali nilipanga niondoke nimuachie nyumba lakini nimeona nikomae hadi kieleweke“.

Mara nyingi Kajala alipokuwa akiulizwa kuhusiana na kuingilia ndoa hii ya mzazi mwenzie amekuwa akikana na kusema kuwa kuwa P Funk ni baba wa mtoto wake na si vinginevyo ingawa video mbalimbali zinavuja zikiashiria ni wapenzi. 

0 Comments

Previous Post Next Post