Magoli ya Samatta yamefufua Matumaini ya KRC Genk kucheza Europa League 2018/19


Baada ya nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayeichezea club ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta usiku wa May 10 2018 kufunga goli lake la kwanza dhidi ya KAA Gent akiwa na KRC Genk toka afanye hivyo kwa mara ya mwisho October 25 2017 katika mchezo dhidi ya Club Brugge, maneno yake baada ya kufunga goli hilo yameanza kutimia.

Mbwana Samatta ambaye alikuwa akipambana na majeraha ya goti miezi kadhaa nyuma, baada ya kufunga goli May 10 2018 dhidi ya KAA Gent na kuinusuru timu yake na kipigo baada ya goli lake kuwa ndio la kusawazishia, alisema kuwa goli hilo litafungua milango ya kufunga zaidi kwa maana alivyikosa kufunga kwa muda mrefu hali yake ya kujiamini ilishuka ukizingatia alikuwa anapambana kurejesha makali yake baada ya kupona goti.

Mbwana Samatta usiku wa May 13 ikiwa ni siku tatu zimepita toka afunge goli, ametimiza maneno yake kwa kuifungia KRC Genk magoli mawili katika ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya Charleroi, Mbwana Samatta ndio alianza kuifungia goli Genk dakika ya 23 na 61, Leandro Trossard dakika ya 34 na Diemerci Ndongala dakika ya 77 wakati goli pekee la Charleroi la kufutia machozi  lilifungwa na Cristian Benavente dakika ya 31.

Ushindi huo sasa wa magoli 4-1 umefufua matumaini ya KRC Genk kupata nafasi ya kucheza hatua ya play off ya UEFA Europa League msimu wa 2018/2019 kwani wamesogea hadi nafasi ya 5 katika timu sita zinazocheza game za play off Ligi Kuu Ubelgiji Genk wakihitaji kupata ushindi tu game yao ya mwisho May 20 2018 dhidi ya Anderletch ili wamalize nafasi ya nne lakini itategemea na matokeo ya mchezo wa KAA Gent dhidi ya Club Brugge kama KAA Gent akipoteza ni faida kwa Genk akishinda.

Mtangazaji wa BBC Swahili Salim Kikeke na Thomas Ulimwengu walikuwepo uwanjani kuangalia game ya Genk dhidi ya Charleroi. 

0 Comments

Previous Post Next Post