Kuna Wasanii Wanatoa Nyimbo Mbaya wanabaki Wanakomaa na Ma-interview tu-Ommy Dimpoz.

Kuna Wasanii Wanatoa Nyimbo Mbaya wanabaki Wanakomaa na Ma- interview tu- Ommy Dimpoz

Wasanii wa muziki Bongo, Ommy Dimpoz amesema kuna baadhi ya wasanii ‘wanatoa’ nyimbo mbaya ila wasanii wanzao wanaogopa kuwaambia.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Yanje’ hilo linatokana wale wanaosema ukweli kuchukiwa siku zote.

“Kuna nyimbo za wasanii wenzangu na nyingine unaona huu wimbo gani na unaona mwana anakomaa na ma-intervie,” amesema.

Amesema ni vigumu kumwambia ukweli msanii mwenzako kwamba wimbo wako si kiwango hicho kutokana tayari ameshawekeza.

“Na siku zote wasema ukweli wanachukiwa, kuna siku niko na washikaji jamaa anamwambia mwana lakini ule wimbo wenu mnaenda ku-shoot video?, mbona ngoma mbaya, nikasema unatoa wapi ujasiri wa kumwambia mtu hivyo,” Dimpoz ameiambia Magic FM.

Utakumbuka kipindi cha nyuma Barakah The Prince aliingia kwenye headlines mara baada ya kudai wimbo wa Ben Pol ‘Tatu’ ni mbaya, hata Godzill aliwahi kufanya kitu kama hicho kwa Nay wa Mitego.

0 Comments

Previous Post Next Post