Kipa Kaseja Kaomba Msamaha Simba 'Nimewaumiza Sana Jana'.


Kwa taarifa yako kama ulikuwa hufahamu, wakati Simba ikitwaa ubingwa bila kupoteza mchezo golikipa wa wakati huo alikuwa ni Juma Kaseja.

Kaseja huyohuyo ameizuia Simba kutimiza ndoto yake ya kumaliza msimu bila kufungwa baada ya kuokoa penati ya Emanuel Okwi dakika ya mwisho katika mchezo wa Simba dhidi ya Kagera Sugar.

“Rekodi tuliweka sisi na mimi nikiwemo, rekodi ya kucheza mechi zote bila kupoteza, namshukuru Mungu yuleyule aliyeweka rekodi ya kucheza mechi nyingi bila kupoteza amevunja rekodi ya watu wengine wasicheze mechi zote bila kupoteza.”
“Lakini vilevile nawaomba msamaha wanasimba nimeishi ndani ya Simba kwa kipindi kirefu nikiwa mchezaji wao leo hii wanaweza kuwa wameumia.”

0 Comments

Previous Post Next Post