Kijana Mwingine wa Kitanzania Auawa Nchini London Kwa Visu.


KIJANA wa Kitanzania kutoka Zanzibar mwenye umri wa miaka 24 (jina bado halijafahamikia) aliyekuwa nchini Uingereza, anadaiwa kuuawa kwa kuchomwa visu na watu wasiojuliakana jana Alhamisi Mei 17, 2018 jioni huko Barking London.

Polisi jijini London wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema walipewa taarifa na mtu wa karibu wa kijana huyo, walipofika walijitahidi kumpatia huduma ya kwanza lakini alipoteza maisha kabla akiwa njiani kupelekewa Hospitali kutokana na majeraha makubwa na kuvuja damu nyingi kufuatia kuchomwa visu sehemu mbalimbali za mwili wake.

Aidha, Polisi wamesema bado hawajamkamata mtuhumiwa yeyote wa mauaji hayo, lakini wanaendelea na uchunguzi wa mauaji hayo ya kinyama na mengine ambayo yameshamiri kwa siku za hivi karibuni yakihusisha kuchomwa visu, milipuko na kupigwa risasi kwa raia.

Kwa mujibu wa chanzo cha www.globalpublishers.co.tz kilichopo London Uingereza, inasemekana kijana huyo ni mtoto wa Mzee Nassor Juma kaka wa Nassra Juma anayefanya kazi katika Idara ya Uhamiaji Zanzibar.
Imearifiwa kuwa, kwa mwaka huu pekee, polisi wamepokea kesi za matukio zaidi ya 60 ya mauaji ambapo 39 ni ya kuchomwa visu na 10 ni ya kupigwa risasi.


Meya wa London, Sadiq Khan amelielezea tukio hilo kuwa ni la kinyama zaidi na limeacha pengo kubwa kwa ndugu na familia huku Mbunge wa Barking, Dame Margaret Hodge kupitia mtandao wa Twitter akitoa salam za rambirambi kwa familia ya marehemu.

CREDIT: BBC NEWS 

0 Comments

Previous Post Next Post