JPM "Ningekuwa na Uwezo Ofisi zote za Serikali Wangekunywa Maji ya Uhuru Peak".


MGULANI, DAR: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli akinywa maji ya Uhuru Peak yaliyotengenezwa na kiwanda cha SUMA JKT, jana Mei 17, katika ufunguzi wa kituo cha uwekezaji cha Suma JKT
-
Rais Magufuli alisema "Mimi kuanzia leo nitakuwa mdau wa maji ya Uhuru Peak nitashangaa sana Waziri wa Ulinzi siku nikimtembelea ofisini kwake nikute anakunywa maji ya aina nyingine au Mkuu wa Majeshi au hata Wastaafu au Mkuu wa Magereza anakunywa maji mengine nitashtuka kidogo, lakini nitashangaa."
-
Aliongeza kuwa "Nayapongeza sana Majeshi yetu, ni bahati mbaya tu sina amri ya kusema sasa maji yote yanayonywewa Serikali yawe yameandikwa hii nembo(Uhuru Peak) kwa sababu huo uwezo sina. Lakini ningekuwa nao huo uwezo ningesema, lakini sisemi."

0 Comments

Previous Post Next Post