Imesalia Pointi 1 Simba kutangaza Ubingwa.Ni baada ya kuichapa Ndanda FC kwa bao 1-0.


Kikosi cha Simba kimeendelea kuunusa ubingwa wa Ligi Kuu kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda FC.

Bao pekee katika mchezo huo limetiwa kimiani na Mshambuliaji wa kimataifa, Mganda, Emmanuel Okwi katika dakika ya 44.

Okwi alifunga bao hilo baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa beki wa kulia, Shomari Kapombe.

Matokeo hayaifanya Simba ifikishe alama 65 kwenye msimamo wa ligi huku Ndanda FC wakisalia kwenye nafasi 15 wakiwa na alama 23.

0 Comments

Previous Post Next Post