Hii ndio sababu ya Rihanna kuvamiwa nyumbani kwake.


Hii ni nyingine ya kuifahamu kutoka kwa staa maarufu  Marekani Rihanna ambapo inaripotiwa kuwa siku ya May 11,2018 alivamiwa katika nyumba yake iliyopo Holly Wood Hills na kijana aliyefahamika kwa jina la Eduardo Leon.

Mashuhuda waliwaambia polisi waliofika nyumbani kwa Rihanna kuwa kijana huyo alifanya hivyo kwa dhumuni la kumuona Rihanna na kukutana naye kimwili kutokana na hisia alizonazo kwa mwanamuziki huyo.

Eduardo Leon mwenye umri wa miaka 26 alifanikiwa kuzima alarm kwenye nyumba hiyo na kufanya uvamizi na pia inasemekana kuwa hii sio mara ya kwanza kwa Eduardo kufanya uvamizi katika nyumba mbalimbali na kuripotiwa kuwa May 4,2018 alifanya uvamizi. 

0 Comments

Previous Post Next Post