Harmonize Afunguka Mazito Kuhusu Kuibiwa Sarah na Baunsa wa Diamond.

Harmonize Afunguka Kuhusu Kuibiwa Sarah na Baunsa wa Diamond

Kwa habari za chini ya kapeti ni kwamba yule mzungu wa Harmonize (Konde boy) Sarah kwa sasa haambiwi wala hasikii kitu kuhusu mwarabu fighter yaani anampenda mpaka kapitiliza ,zile pesa alizokuwa ana muhonga Harmonize kwa sasa kwa kiasi kikubwa amezihamishia kwa mwarabu fighter na gharama za gym kwa kiasi kikubwa yeye ndiye anazisimamia.

Sarah amepunguza mapenzi kwa kiasi kikubwa na Harmonize kilichobaki anahangaikia tu penzi la mwarabu fighter ili aweze kutuliza roho yake.

Kitu ambacho mpaka sasa kinachofanya ugumu wa couple hiyo kusimama ni kutokana na Harmonize kuwa mtu wa karibu saana na Diamond Platnumz ambaye pia ndiye anayemuweka mjini mwarabu fighter na siku zote ukitaka kumkwaza Diamond au ukitaka kumkwaza Harmonize basi mtu amkwaze mmoja wapo yani Diamond wanapendana sana kama mtu na kaka yake.

Kwa hiyo mwarabu fighter anaogopa kibarua kuota nyasi kama akifanikiwa kumpindua Harmonize . 

0 Comments

Previous Post Next Post